UTALII WETU

                      JE WAJUA? 

UTALII NI NINI?
Utalii ni kitendo cha watu au mtu kuondoka kwenye mazingira yake ya kila siku (mfano, mahali unapoishi au kufanya kazi) na kufanya safari au matembezi ya muda sehemu nyingine kwa nia ya kupumzika au kufanya kazi. Shughuli atakazozifanya ikiwa ni pamoja na kuangalia mazingira n.k, kutumia miundombinu (barabara, nyumba za kulala wageni n.k) atakayoitumia kukidhi mahitaji yake nje ya mazingira yake ya kila siku wakati akiwa safarini humfanya mtu huyo aitwe MTALII.

Hivyo kufanya shughuli nzima inayofanyika iitwe UTALII. Na ili mtu atambulike kama mtalii kuna mambo matatu muhimu nayo ni;
 a) Kutoka sehemu moja kwenda nyingine
b) Lengo la matembezi hayo 
c) Muda wa kukaa katika sehemu husika, unatakiwa ukae si chini ya masaa 24 na si zaidi ya mwaka. 

KWA NINI KUTALII? 
Kuna sababu mbili kuu: 
A) MSUKUMO KUTOKA NDANI Mtu amechoka kukaa kwenye mazingira yake ya kila siku hivyo kuhitaji: Kuyaondoka kwa muda mazingira yake ;

  •  Kwenda kupumzika 
  • Kucheza 
  • Fursa za kielimu 
  •  Kuimarisha undugu wa kifamilia 
  •  Mahusiano ya kijamii 
  •  Kuitosheleza nafsi yake 
  • Manunuzi n.k    
  •                                                                                                                                                         B) MVUTO KUTOKA NJE § Umashuhuri au sifa za mahali husika § Fahari § Utofauti na mahali pengine n.k
  •  
  •  

No comments:

Post a Comment

 

CONTACT US



FOLLOW US
BLOGGER FOUNDER: CHALII High Definition Technology
STUDIO LOCATION:UHINDINI STREET
E-mail address;frank4rl@gmail.com
Tel. no. +25517775181/+255785783949

Blogroll

About Us