Rais John Pombe Magufuli leo jumatatu July 16,2018 amezindua ujenzi wa chuo cha uongozi Julius Nyerere kilichopo Kibaha Mkoani Pwani.
Akizungumza leo Katibu wa Itikadi na uenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole amesema chuo hicho kitakuwa kikiwaandaa viongozi na kuwapika makada wa chama hicho na vyama vinginevyo vilivyoshiriki harakati za ukombozi kusini mwa bara la Afrika.
''Hiki ni chuo cha CCM chenye lengo la kuwanoa viongozi wa chama kama ilivyokuwa miaka ya nyuma kwa hiyo tunatarajia darasa la mwanzo kabisa kuanza 2020 kitakapokamilika'' Huku Mwenyekiti wa chama hicho CCM , Rais John Pombe Magufuli akisema "CCM ni chama Tawala na kitaendelea kutawala milele na milele,wanaohangaika watapa tabu siku zote,chama hiki kipo na kitaendelea kuleta maendeleo kwa ajili ya watanzania.Hakuna mbadala ni CCM hadi milele"
JULY 11,2018
NHIF KUWACHUKULIA HATUA WANAOTIBIWA KUPITIA KUPITIA KADI ZA WATU WENGINE
Kumekuwa na tabia isiyokuwa ya kiungwana kwa baadhi ya wanachama wa NHIF kwenda kuwatibu ndugu zao ambao si wanachama kupitia Kadi zao, Meneja wa NHIF mkoa wa Ruvuma Abdiel Mkaro amesema atawachukulia hatua za kisheria wanaotibiwa kupitia kadi za ndugu zao wakati sio wanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya Afya,huku akielezea mkanganyiko unaojitokeza kwa mteja anayetibiwa kwa kadi isiyo yake pindi anapofariki,huku mkuu wa wilaya ndugu Cosmas Nshenye akiwahimiza madaktari kutoa huduma nzuri kwa wateja wa bima ya Afya.
JULY 8,2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli akipokea Ndege Mpya
Tazama ujionee ndege hii aina ya
Boeing 787 Dreamliner inavyotengenezwa. Ndege hii ina uwezo wa kubeba watu zaidi ya 240 na ina uwezo wa kwenda masafa marefu.
JULY 7, 2018
Kwa mara ya kwanza Dr. Mwigulu Nchemba tangu Rais John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko madogo katika baraza lake la Mawaziri ikiwemo kumuondoa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr Mwigulu Nchemba na nafasi hiyo kuchukuliwa na Kangi Lugola.azungumzia Tetesi zilizosambaa kuwa anataka kujiuzuru Ubunge katika jimbo lake la Iramba Magharibi, Dr. Mwigulu Nchemba aliyasema hayo katika mkutano na wananchi wake ulofanyika katika Jimbo lake.
“Nimesikiasikia kwenye mitandao kwamba Ooooh! Nitaacha na Ubunge, uliona wapi mchezaji asajiliwe kwenye club yake ya kuchezea akaonekana team ya taifa alafu siku akiondoka team ya taifa aseme hata club yenu sichezei. Hili sio jambo la ugomvi na wala msipate shida. Nilipopata fursa ile kuna mambo mlikuwa mnakosa kwasababu muda mwingi nilikuwa na majukumu ya kitaifa
No comments:
Post a Comment