ANGA ZA KIMATAIFA

 

JULY 16,2018

Mbunge azuiwa kuingia hotelini Kenya kwa sababu ya cheti cha ndoa

 

  Bi Catherine Waruguru anasema haki zake za kimsingi zilikiukwa baada yake na mumewe kuzuiwa kuingia katika hoteli moja nchini humo kwa kukosa cheti cha ndoa.

Mbunge huyo ametishia kuishtaki hoteli hiyo ya mjini Kericho, eneo la Bonde la Ufa akisema alidhalilishwa.
Hoteli hiyo imeweka ilani kwamba mwanamume na mwanamke hawawezi kuruhusiwa katika chumba kimoja iwapo hawajaoana.
Lakini mbunge huyo anasema wanandoa wengine waliruhusiwa kuingia bila kuitishwa cheti cha ndoa, na kwamba walifanya kila juhudi kuthibitisha kwamba walikuwa mume na mke ingawa hawakuwa na cheti cha ndoa.

 


  Je Trump na Putin watajadili nini katika mkutano wao?

Rais wa Marekani Donald Trump na wa Urusi Vladmir Putin muda mchache ujao watakutana kwa mazungumzo, katika makazi ya Rais wa nchi hiyo mjini Helsinki, ambao ni mkutano wao wa kwanza kabisa kuwakutanisha pamoja.
Mpaka sasa hakuna ajenda yoyote ya mkutano huo, ambao utahudhuriwa tu na watafsiri wao.
Aidha licha ya mkutano huo kutotegemewa sana, lakini wanaweza kuonesha dalili mpya za kuanza kwa awamu mpya ya mahusiano kati ya Washngton na Moscow, baada ya kufarakana kufuatia Urusi kuitwaa kwa nguvu Crimea.
Aidha wachunguzi wa mambo wanadhani pia kuna hatua inaweza kupigwa katika kuumaliza mzozo wa Syria na pia mazungumzo kuhusiana na masuala ya Nyuklia.

 

JULY 14, 2018

Barrack Obama: Kufanya ziara ya kibinafsi nchini Kenya Jumapili

 

Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuwasili nchini Kenya siku ya Jumapili katika ziara ya kibinafsi.

 

11JULY 2018

 Samuel Umtiti mchezaji aliyewafikisha Ufaransa fainali kwa kuwafunga Ubelgiji nusufainali

Ufaransa watakutana na mshindi kati ya England na Croatia kwenye fainali ya Kombe la Dunia nchini Urusi baada ya kuwashinda majirani wao Ubelgiji kwenye nusufainali mjini St Petersburg.

Mechi ya fainali itachezwa Jumapili uwanjani Lzhiniki mjini Moscow saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.
Ubelgiji wamesalia na mechi moja ya kuamua atakayemaliza wa tatu, mechi ambayo itachezwa Jumamosi.
Bao pekee la mechi ya nusu fainali lilifungwa na beki Samuel Umtiti baada ya kona iliyopigwa na Antoine Griezmann.

 

  Polisi nchini India watakiwa  kupunguza uzito vinginevyo wafukuzwe kazi

 Sio kawaida kuwaona Polisi nchini humo wakifanya mazoezi kuondokana na tatizo la uzito mkubwa.


Maafisa wa juu wa kikosi cha KSRP kimekuwa kikiamriwa kuwatambua maafisa wenye uzito mkubwa na kuwaweka katika mpango wa kufanya mazoezi ili kupunguza uzito
''Tumeanza kazi ya kuwafuatilia maafisa kwa kupima sukari na vipimo vingine miezi sita iliyopita.Hatua hii mpya ya kusimamishwa kazi ni kitisho kwa wale wasiojali afya zao''.Rao Bhaskar Rao amesema alichukua uamuzi huo baada ya maafisa zaidi ya 100 kupoteza maisha katika kipindi cha miezi 18 iliyopita kutokana na maradhi yaliyo na uhusiano na mtindo wa maisha Rao ameongeza kuwa maafisa walikuwa wakila zaidi vyakula vya kukaanga, walikuwa wakivuta sigara, kunywa pombe na hawakuwa wakifanya mazoezi.
Mafunzo ya kuogelea, Yoga na michezo mingine imeanza kutolewa kwa maafisa.
''Mafunzo yameanza kutolewa baada ya kufanyika vipimo na mazoezi yatafanyika kwa kuzingatia ushauri wa madaktari'', alieleza Rao

 

 10JULY 2018

Merkel na Li watafuta ushirikiano zaidi wa kibiashara

 Ujerumani yatafuta ushirikiano zaidi na China

Merkel amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushirikiano unaoweza kutegemewa kati ya China na Ujerumani hasa wakati huu ambapo kuna ukosefu wa usalama duniani. Kwa upande wake, Li amemueleza Merkel kuwa China kwa hakika inataka kuuendeleza uhusiano utakaozinufaisha pande zote mbili.Kansela huyo wa Ujerumani amesema nchi zote mbili zinataka kudumishwa kwa sheria za shirika la biashara duniani WTO, na amejadili kwa kina na Li kuhusu suala la kuwa na biashara huru zaidi. Kumekuwa na wasiwasi miongoni mwa maafisa wa Umoja wa Ulaya kuwa kampuni za China zinapata urahisi kuwekeza Ulaya kuliko jinsi kampuni za Ulaya zinavyoweza kuwekeza China.




9 JULY 2018

 Thailand

Uokoaji wa watoto waliokwama pangoni  waendendelea

Watoto nane wameokolewa wakiwa hai kati ya 12 waliokwama ndani ya pango lililojaa maji huko nchini Thailand,huku jitihada za uokoaji zikiwa zimesitishwa kwa muda katika kazi hiyo inayotajwa kuwa ni hatari kwa waokoaji pia kwani tayari mzamiaji mmoja amefariki dunia katika kazi hiyo.
Imekuwa ni habari yenye simanzi kwa dunia, ambapo wazamiaji kutoka nchi mbali mbali wamewasili Thailand,kusaidia kazi hiyo,huku wazazi wa watoto hao wakiwa katika hali ngumu na kuomba kila linalowezekana lifanyike kunusuru maisha ya watoto wao.
Watoto hao wa kiume walikwama mapangoni humo tangu June 23 huku uokoaji wao ukiwa ni wa hatari na wenye vikwazo vingi kwa maisha ya waokoaji.
Awamu nyingine ya uoakoji watoto hao na kocha wao walioingia ndani ya pango hilo kufanya utalii inatarajiwa kuanza tena leo siku ya Jumatatu ambapo kazi hiyo ilisimamishwa kwaajili ya maandalizi Zaidi ya vifaa vya hewa.
Wavulana 6 kati ya 12 waliokwama pangoni Thailand waokolewa
Njia ya kuwaokoa vijana 12 waliokwama kwenye pango inatafutwa
Mamilioni ya lita za maji yamekwisha kutolewa kutoka ndani ya pango hilo,ili kurahisisha kazi ya uokoaji.

July 7,2018

 Rais Salva Kiir kumteua tena Riek Machar kuwa makamu wa Rais

 SALVA  KIIR

                           Riek Machar

Wanasiasa wa Sudan Kusini hatimaye wamechukua hatua zaidi ambayo inaonekana ndio ya kuelekea kumaliza vita vya miaka mitano vya wenyewe kwa wenyewe kwa kutagaza makubaliano ya ugavi wa madaraka kati yao.
Rais Salva Kiir, atamrejesha tena kiongozi wa wapiganaji, Riek Machar, kuwa makamo wake wa rais.
Pia kundi la Bwana Machar, litapewa nafasi katika baraza la mawaziri na bungeni.
Mazungumzo ya kupata maelewano zaidi, yanatarajiwa kufanyika nchi jirani katika siku chache zijazo.
Rais Kiir alimfuta kazi Bwana Machar mwaka hapo 2013, akimshutumu kwamba alipanga njama ya kupindua serikali.
Maelfu ya watu wamekufa katika mzozo wa vita vya kisiasa uliofuata.
Mwezi uliopita, pande hizo mbili zilitia saini mkataba mwengine wa kusitisha mapigano baada ya ile ya awali kufeli.


JULY  6,2018

Mwanamume akwama baada ya lami kuyeyuka barabarani Newcastle, Uingereza

Kijana huyo wa miaka 24 aliwapigia maafisa wa huduma za dharura kupitia nambari 999 baada ya mguu wake wa kushoto kukwama barabarani.
Mguu wake ulikuwa umetumbukia hadi karibu pajani katika barabara moja ya pembeni eneo la Heaton, Newcastle.Hali hiyo ilisababishwa na jua kali ambalo limekuwa likiwaka eneo hilo.

 

No comments:

Post a Comment

 

CONTACT US



FOLLOW US
BLOGGER FOUNDER: CHALII High Definition Technology
STUDIO LOCATION:UHINDINI STREET
E-mail address;frank4rl@gmail.com
Tel. no. +25517775181/+255785783949

Blogroll

About Us